
Katika jitihada za
kuufanya mkoa wa Dodoma kuwa wa kijani
imeelezwa kuwa changamoto kubwa
inayowakabili wananchi ni ukosefu
wa maji hasa maeneo ya vijijini.
Hayo yameelezwa na
mkurugenzi wa shirika linalojihusisha na uhifadhi wa mazingira mkoani Dodoma la
LEAD FOUNDATION Bwana Njamas Chiwanga wakati akizungumza na kituo hiki.
Bwana njamasi
amesema ukosefu wa maji katika maeneo ya vijijini imekuwa changamoto kubwa
hivyo suluhisho ni kuepuka kukata miti ya asili kutokana na miti hiyo
kutokutumia maji mengi.
Shirika hilo
limeanzisha kampeni ya KISIKI HAI lengo ni kuhamasisha wananchi katika mkoa wa
Dodoma kuepuka kukata miti ya asili kwani miti hiyo ina kivuli cha kutosha huku akiwataka wale wenye uwezo wa kupanda
miti ya kisasa kuendelea kupanda ili kuboresha mazingira.
Kwa upande wake
afisa masoko wa shirika hilo bwana Godlove Kihupi amesema tangu walipoanza kampeni hiyo mwaka 2017 wamefanikiwa kwa
asilimia 30 mpaka sasa.
Shirika la LEAD
FOUNDATION linashirikiana na shirika la kimataifa la uholanzi la just digit
lengo ni kuhamasisha wakazi mkoani Dodoma utunzaji wa miti ya asili ambapo tayari wamewafikia watu 48,000 lengo
ni elimu hiyo kuwafikia wakazi 180,000.
Na
Benard Filbert DODOMA
FM
Comments
Post a Comment