Ili kudhibiti
uharibifu wa uoto wa asili ambao unasababishwa na shughuli za kibinadamu afisa
maliasili katika halimashauri ya jiji la Dodoma amesema tayari wameanza kutoa
elimu kwa wananchi katika Kata zote.
Akizungumza na Dodoma FM Afisa maliasili VEDASTUS
MILINGA amesema kutokana na mji kupanuka wananchi watalazimika
kuharibu uoto wa asili hivyo wameona ni vyema kuanza kutoa elimu kwa wananchi
kwa lengo la kudhibiti kuendelea kukata uoto wa asili hali ambayo imepelekea
Dodoma kuwa jangwa.
Aidha amesema kutokana na uoto wa asili kuwa na umuhimu wamefanikiwa
kuanzisha doria kwa kupita kila kanda lakini
pia wanashirikiana na na TFS katika
kudhibiti uharibifu wa uoto pamoja na kutoa elimu kwa wananchi.
Kwa upande wao
baadhi ya wananchi wamesema kinachopelekea uharibifu wa uoto ni wananchi
kujipatia kipato kwa njia ya uchomaji mkaa.
Ili kufikia azma
ya serikali ya Dodoma kuwa ya kijani afisa maliasili kwa kushirikiana na afisa
misitu wanafanya jitihada kwa kupanda miti ya asili ambayo itasaidia kuondoa
jangwa katika jiji la Dodoma.
Na,Mindi Joseph
DODOMA
FM
Comments
Post a Comment