SERIKALI
imesema hadi kufikia mwaka 2017/18 tayari imekwisha lipa deni la Shilingi
billion 309.77 kati ya deni la shilingi bilion 413.96 la malimbikizo ya mafao
ya wastaafu wanaolipwa kupitia Bank kuu.
Malipo
hayo ni sawa na asilimia 74.83 ya malipo ya deni hilo huku ikitabainisha kuwa
hadi sasa imekwisha lipa jumla ya Shilingi Tirion 1.36 ikiwa ni deni
lote la malimbikizo ya michango ya wastaafu kupitia mifuko ya hifadhi za jamii.
Hayo
yameelezwa na Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Wazee,Vijana na
Watu wenye ulemavu Mh.Jenista Mhagama Jijini Dodoma wakati akizindua mpango wa
mikopo ya wastaafu iliyoandaliwa na Bank ya NBC.
Mbali
na kuipongeza Bank hiyo kwa mpango huo Mhagama amesema kama Serikali sasa
imeamua kulipa madeni ya wastaafu ili kuwapa mwanya wa kutumia mafao yao kupata
mikopo.
Waziri
Mhagama ameongeza kuwa mara baada ya kuunganishwa kwa mifuko ya hifadhi ya
jamii Serikali itahakikisha inatengeneza mfumo utakaowezeha wastaafu wote
wanapata mafao yao pasi kuwepo kwa usumbufu na vikwazo vya kuchelewa kwa mafao
yao.
Kwa
upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Bank ya NBC Tanzania Theobald Sabi ametaja
sababu zilizowapelekea kuanzisha mikopo hiyo kwa wastaafu kuwa ni pamoja na
kuwasaidia kuendesha maisha yao mara baada ya kustaafu.
Nao
baadhi ya wastaafu waliohudhuria katika uzinduzi huo wameipongeza Bank ya NBC
na kusema sasa wamepata nguvu mpya ya kuendeleza maisha yao.
Na MARIAM MATUNDU CHANZO:DODOMA FM
Comments
Post a Comment