
Serikali kupitia
Wizara ya Afya imesema haina changamoto ya upatikanaji wa dawa wala fedha kwa ajili ya vifaa tiba pamoja na
vitendea kazi.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mh. FAUSTINE NDUNGULILE amebainisha hayo na kueleza kuwa changamoto iliyopo ni
kwa watoa huduma kuwa na mawazo ya kipindi cha nyuma ya ukosefu wa vifaa.
Naibu waziri huyo ameyasema hayo wakati akizungumza na Dodoma FM juu ya uwepo wa changamoto ya upatikanaji wa dawa pamoja na vifaa tiba nchini.
Mh Ndungulele amesema kuwa mara nyingi wizara
imekuwa ikipata taarifa ya kuwepo kwa changamoto ya ukosefu wa baadhi ya vitu
hivyo lakini wanapofuatilia hugundulika kuwa baadhi ya watoa huduma hawafuatilii vitu hivyo MSD.
Katika hatua nyingine Ndungulele amesema
kumekuwa na ongezeko la watu katika Mkoa wa Dodoma kutokana na serikali kuhamia hivyo serikali inatambua kuwepo kwa
changamoto ya Chumba cha kuhifadhi maiti hivyo katika bajeti inayokuja Wizara hiyo imeweka kipaumbele katika suala hilo.
Akizungumzia
gharama za matibabu Ndungulile amesema serikali imedhamiria kuja na mfumo wa
bima ya afya kwa mwananchi mmoja mmoja ili kila mwananchi aweze kufaidika na
bima ya afya.
Na
Phina Nimrod Dodoma FM
Comments
Post a Comment