Kufuatia kuwepo kwa taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya
kijamii ambazo zinaonyesha makosa ya
uchapishaji wa kitabu cha kingereza cha darasa la tatu waziri wa elimu sayansi
na teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama
kuwasaka watu wanaosambaza taarifa hizo mitandaoni.
Hivi karibuni katika mitandao ya kijamii kumekuwepo na taarifa
zinazoonesha makosa katika vitabu vya masomo ya shule ya msingi Taarifa hizo
zimepelekea mbunge wa viti maalumu Martha Mlata kuomba ufafanuzi wa serikali
kuhusua vitabu hivyo ambapo leo waziri wa elimu sayansi na teknolojia Prof.
Joyce Ndalichako ametolea ufafanuzi suala hilo.
Prof. Ndalichako amesema kuwa kitabu cha kiingereza cha darasa
la tatu kinachosambaa mtandaoni kilikuwa na makosa na kilirekebishwa huku
wahusika wakichukuliwa hatua lakini kitabu kinachoonesha picha inayoonesha sehemu
za mwili wa mwanadamu ni kitabu ambacho hakitambuliki na serikali hivyo wanaokisambaza
watafutwe na wachukuliwe hatua.
Kitabu hicho kilisambaa mitandaoni jana na moja ya kurasa zake inaonyesha sehemu za mwili wa binadamu kwa njia tofauti ambapo
shingo inaonyesha kifua, paja (kiuno), kichwa (nyusi), sikio (shingo) na sehemu
nyingine mbalimbali za mwili.
Na,Mindi joseph Dodoma FM
Comments
Post a Comment