Kwa
mujibu wa tafiti zilizofanywa na Jeshi la Polisi Nchini imebainika kuwa ajali
za barabarani zinasababishwa na vyanzo vikuu vitatu ikiwemo vya kibinadamu 76%, vya kiufundi 16% na vya kimazingira kwa asilimia 8.
Waziri
wa mambo ya ndani ya Nchi Dr. Mwigulu Nchemba ameyabainisha hayo leo Bungeni
Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Tabora Mjini Mh. Emmanuel Adam
Sony alietaka kujua Serikali ina mkakati gani kuhakikisha ajali za kizembe
zinazosababishwa na baadhi ya askari Polisi zinakomeshwa.
Dr.
Mwigulu amesema katika vyanzo vya kibinadamu kuna uzembe ambao umekuwa
ukijitokeza hasa kwa waendesha pikipiki ambao wamekuwa na uelewa mdogo juu ya
sheria za usalama barabarani na kutokana na sababu hizo waendesha pikipiki
hujihisi wana makosa wakati wowote wanapoendesha vyombo vyao wakihofia
kukamatwa na Polisi.
Amesema
ni wajibu wa askari Polisi kuhakikisha kuwa sheria zinafuatwa na waendesha pikipiki
wanapaswa kutambua hilo na kutimiza wajibu wao wa kufuata sheria badala ya kumkwepa
askari kutokana na makosa yanayojitokeza .
Akielezea
juu ya kima cha faini anayopaswa kutozwa dereva bodaboda Waziri Mwigulu amesema
swala hilo linatarajiwa kupitishwa kupitia bajeti ya Wizara ya fedha na mipango
ili kutofautisha faini wanayotozwa madereva bodaboda, mabasi pamoja na vyombo
vingine vya usafiri.
Na Pius Jayunga Dodoma FM
Comments
Post a Comment