Waziri mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa amesema Serikali ipo katika
mkakati wa kupanga bajeti ya utoaji wa huduma ya chakula kwa wanafunzi katika
shule za sekondari za kutwa zikiwemo pia shule za msingi kote Nchini.
Waziri mkuu Kasimu
Majaliwa ameyasema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma katika kikao cha 26 mkutano
wa 11 katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa waziri mkuu wakati
akijibu swali la Mbunge wa Temeke Abdalha Mtolea aliehoji ni lini Serikali
itabadilisha sera ya elimu ili utoaji wa huduma ya chakula kwa wanafunzi
itambulike rasmi.
Waziri Mkuu amesema Tanzania
ina jumla ya shule milioni 17 idadi ya shule za sekondari zikiwa 3547 na kwamba
serikali imeanza kutoa huduma hiyo kwa wanafunzi wa shule za sekondari za kutwa
huku zoezi hilo likiendelea kuratibiwa ili kuwafikishia huduma hiyo wanafunzi
wa shule za msingi kote nchini.
Mh. Kasimu Majaliwa
amesema baada ya Serikali kuanza kutoa elimu bure imesaidia watoto wengi kupata
elimu na kueleza kuwa ni jukumu la wazazi
na walezi kushirikiana na Serikali hasa katika kufanikisha upatikanaji wa
huduma ya chakula kwa wanafunzi.
Baada ya kukamilika
kwa kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri mkuu wabunge wameendelea na
maswali ya kawaida ambapo Mbunge wa viti maalumu Zainabu Mdolo Amiri amehoji ni
lini Serikali itapunguza gharama ya gesi kwa matumizi ya nyumbani ili
kuwawezesha wanachi wengi kupata huduma hiyo na kuondokana na matumizi ya kuni
na mkaa.
Akijibu swali hilo
Naibu Waziri wa nishati Mh. Subira Mgaru amesema mikakati ya kuunganisha gesi
majukumbani inaendelea na katika awamu ya kwanza mradi huo utapita katika
maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam na Mtwara kisha kusambaza huduma
hiyo katika maeneo yote Nchini.
Na
Piud Jayunga Bunge/Dodoma FM
Comments
Post a Comment