
Jumla ya wazee 15,854 walio na zaidi ya miaka 60
kutoka kata mbalimbali za mkoa wa Dodoma wanatarajia kupewa vitambulisho
maalumu vitakavyowasaidia kupata matibabu bure katika hospitali mbalimbali
zilizopo hapa nchini.
Hayo
yamebainishwa leo na Mganga mkuu mkoa wa Dodoma Dkt Hamad Nyembea wakati
akizungumza na kituo hiki ambapo amesema kuwa wazee kutoka katika kata 33
wametambulika ili kupatiwa vitambulisho kwa ajili ya kupatiwa matibabu bure.
Amesema
kuwa lengo la kutoa vitambulisho hivyo ni kuhakikisha wazee wanatambulika na
kupewa fursa kwenye shughuli mbalimbali za kimaendeleo ikiwa ni pamoja na
kupatiwa matibabu na kwamba wazee 1,118
tayari wamekwishapigwa picha kwa ajili ya zoezi hilo huku wengine 355
kutoka kata ya Mkonze mkoani hapa tayari wamepatiwa vitambulisho hivyo.
Aidha
ameongeza kuwa awali wazee katika maeneo mbalimbali walikuwa wakipata taabu
pindi wanapohitaji matibabu na kupitia vitambulisho hvyo vitawasaidia katika
nyanja mbalimbali katika maisha yao na kwamba kuanzia wiki ijayo zoezi hilo
litaendelea katika maeneo mengine mkoani hapa.
Kwa
upande wao baadhi ya wazee waliopatiwa vitambulisho hivyo wameishukuru serikali
kwa hatua hiyo huku wakiitaka serikali kuhakikisha inatoa huduma za uhakika
kwani ipo changamoto ya kokosa huduma kikamilifu kwa wazee hao kama kutakiwa
kununua dawa katika maeneo mengine ya nje ya hospitali wanazokwenda licha ya kupewa vitambulisho hivyo.
Ikumbukwe
kuwa wiki iliyopita waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za
mitaa Seleman Jafo akiwa katika zoezi la utoaji wa vitambulisho hivyo kwa wazee
wa kata ya Mkonze alitoa muda wa siku 34 kuhakikisha kila mkoa unatoa taarifa
za kuwatambua wazee kwani jambo hili limekuwa likipigiwa kelele kwa mda mrefu
bila mafanikio na watakaoshindwa kutekeleza serikali haitasita kuwachukulia
hatua.
NA
ALFRED BULAHYA DODOMA
FM
Comments
Post a Comment