Katika kudai haki
ya msingi ya kumjua mzazi wa upande wa pili baba au mama katika familia
walengwa ambao ni watoto wazawa wameshauriwa kubuni mbinu sahihi
na kufuata taratibu ili kufanikisha lengo pasipo kupata madhara.
Ushauri huo unakuja
baada ya baadhi ya familia kuwa na migogoro inayohusisha watoto na wazazi wao
chanzo kikiwa ni pale mtoto anapoanza kudai haki yake ya msingi ya kutaka
kumjua mzazi wake wa upande wa pili wa kike au wa kiume jambo ambalo huzua
tafrani.
Akizungumza na
Dodoma FM ofisini kwake mwanasheria kutoka National Attorney Advocates jijini
Dodoma Bwana PAUL KUSEKWA amesema
migogoro katika familia inayohusu watoto kudai kumjua mzazi wa upande wa pili
bado ni tatizo hivyo amewaomba watoto kutumia njia sahihi za kupata ufumbuzi
pasipo kuleta madhara huku akiwaomba nao wazazi husika kuwaonesha watoto wao
wazazi wa pili kwani ni haki yao.
Amesema kudai haki
kwa kutotumia taratibu kunaweza kuzua mijadala mingine na mikubwa ikiwemo kupoteza
haki yako ya msingi kabisa huku akisema swala la kwa nini mzazi hataki
kumwonyesha mtoto wake baba au mama inatokana na historia yao tangu kukutana.
Aidha amesema mtoto
kukosa haki ya kuwajua wazazi wa
pande zote mbili kunachangia kukosa
mahitaji yake muhimu kama elimu chakula na malazi,huku akisema asilimia kubwa ya migogoro inayoendelea
katika familia ya kumdai mzazi wa pili inaonesha wazazi wa kike wanaongoza
kulalamikiwa kwa kutowaonesha watoto wao wazazi wao wa kiume.
Na
RWEIKIZA KATEBALIRWE
DODOMA FM
Comments
Post a Comment