
Wazazi wametakiwa
kuachana na mazoea ya kupata watoto kabla ya kuingia kwenye mkataba wa ndoa ili
kuwapa haki watoto wao.
Hayo yamezungumzwa
na wakili wa kujitegemea lakini pia ni mwanaharakati wa haki za binadamu
Tanzania Bw. JOBA KAMBOLE wakati akizungumza
na Dodoma Fm ambapo amesema kuwa jambo hili limekuwa likichukuliwa kwa mazoea
hali ambayo hupelekea watoto wa nje ya ndoa kukosa haki ya urithi.
Amesema kwa mujibu
wa sheria ya mtoto namba 21 mwaka ya 2009 inasema watoto wote wanahaki sawa na
wanahaki ya kupata mirathi bila ubaguzi na.
kwa upande wao
baadhi ya wananchi wamewataka wazazi kuliangalia swala hilo kwa kufanya maamuzi
sahihi ya kuolewa au kuoa pindi wanapohitaji kupata watoto ili kutowanyima
watoto wao haki zao za mirathi.
Changamoto ya
ongezeko la watoto wa mitaani limekuwa likichochewa zaidi na wazazi kutokana na
kutozingatii maadili ya dini na kupelekea kuzaa watoto nje ya ndoa .
Na
ANIPHA RAMADHAN
DODOMA FM
Comments
Post a Comment