Waziri
wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu amesema Serikali
kupitia wizara ya afya imekamilisha maandalizi ya kuwezesha watu kujipima wao
wenyewe maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa kutumia mate.
Waziri
Ummy ameyasema hayo leo katika mkutano wa 11 kikao cha 41 cha Bunge la Jamhuri
ya muungano wa Tanzania wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Jimbo la
Mtambulie Masoud Abdalla Salim aliehoji mkakati wa Serikali kutambua watu
wanaoathirika na maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Waziri
Ummy amesema mkakati wa Serikali uliolenga kuwapa watu fursa ya kupima
maambukizi ya virusi vya ukimwi
umekamilika na tayari mwanasheria mkuu wa Serikali amekwisha kuandikiwa
barua ili kuleta mabadiliko madogo ya sheria itakayoruhusu mtu kujipima
maambukizi ya virusi vya ukimwi na kuyapata majibu ndani ya dakika 15.
Nae
Waziri ofisi ya Waziri mkuu sera, Bunge, kazi, ajira na wenye ulemavu Mh.
Jenista Mhagama amesema baada ya kuzinduliwa kwa takwimu za ukimwi kwa mwaka
2017 imesaidia kujua hali ya ukimwi kutoka Mkoa mmoja hadi mwingine na kwamba
tume ya kudhibiti ukimwi Nchini TACAIDS imepewa jukumu la kuhakikisha kila Mkoa
unatengeneza mkakati wa kutokomeza maambukizi hayo kulingana na takwimu za mkoa
husika.
Kwa
upande wake naibu Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dr.
Faustine Ndugulile amesema takwimu za maambukizi ya virusi vya ukimwi Nchini
ziko sahihi na huratibiwa na Serikali kupitia taasisi ya TACAIDS pamoja na
wizara ya afya kitengo cha ukimwi ambao ndio waratibu wakuu wa takwimu hizo.
Na Pius Jayunga BUNGE/Dodoma FM
Comments
Post a Comment