
Watahiniwa wa Kidato cha Sita wapatao 1828 katika
halimashauri ya jiji la Dodoma kwa mwaka
2018 wamehimizwa kutumia maarifa waliyoyapata darasani katika miaka miwili ili
kupata ufaulu mzuri.
Rai hiyo imetolewa na afisa elimu sekondari Bwana ABDALLAH MEMBE wakati akizungumza na Dodoma FM juu utaratibu unavyokwenda kwa watahiniwa hao ambao wameanza mitihani mapema hapo jana.
Bwana Abdallah amesema
wanafunzi wanapaswa kutumia kile walichojifunza darasani katika kujibu maswali
kwa lengo la kupata matokeo mazuri pamoja na kuongeza ufaulu nchini.
Amebainisha
kuwa wameweka ulinzi wa kutosha katika
kusimamia mitihani hiyo ili kuepusha udanganyifu ambao unaweza kujitokeza
katika kusimamia mitihani hiyo.
Aidha amebainisha changamoto mbalimbali za kiutendaji
ambazo zimejitokeza ikiwemo kukosewa kwa jina la mtahaniwa na kupelekea kuanza kurekebisha pamoja na
wanafunzi kupata shida kidogo ikiwa ni kupata tatizo la akili na kushindwa
kuona vizuri.
Watahiniwa 1828 Wananafaya mitihani ya taifa
ya kidato cha sita katika jiji la Dodoma na vituo vikiwa 16
ambapo vituo vya sekondary ni 13 na vituo vya ualimu ni 3.
Na,Mindi
Joseph Dodoma FM
Comments
Post a Comment