Idara ya uhamiaji
mkoani Dodoma imewataka wananchi wote wanaoishi katika jiji la dodoma kufuata sheria
,kanuni na taratibu za uhamiaji kama
inavyotakiwa ili kuendelea kutokomeza wimbi la uwepo wa wahamiaji haramu.
Hatua hiyo imekuja
kufuatia mkoa wa Dodoma kupandishwa hadhi ya kuwa jiji na Rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza kwenye
maadhimisho ya siku ya muungano wa Tangnyika na Zanzibar ambao huadhimisha kila
mwaka ifikapo april 26.
Akizungumza leo na
taswira ya habari ofisini kwake afisa uhamiaji mkoa wa Dodoma Bwana Peter Kundi
amesema kuwa tayari wamejipanga kuimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali
ikiwemo nyumba za kulala wageni ,maeneo ya mikusanyiko ya watu na katika
barabara zinazoruhusu watu kuingia na kutoka mkoani hapa kwa lengo la kupambana
na wahamiaji haramu ambapo wamekuwa wakitajwa kuwa chanzo cha uhalifu hapa
nchini.
Katika hatua
nyingine amewataka wananchi kuwa wazalendo kwa kuacha kuwahifadhi wahamiaji
haramu katika maeneo mbalimbali na badala yake kujenga desturi ya kutoa taarifa
kwa vyombo husika pindi wanapobaini uwepo wa wahamiaji haramu ili kuendelea
kulinda usalama wa nchi kwani jukumu hilo ni la kila mwananchi.
NA
ALFRED BULAHYA DODOMA
FM
Comments
Post a Comment