Katika kuadhimisha
siku ya Historia Duniani Imeelezwa kuwa moja ya changamoto inayoikabili jamii
ya leo hasa katika karne hii ya 21 ni kushindwa kutunza kumbukumbu ya mambo
yaliyopita na kuyaweka katika maandishi kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Hayo yameelezwa na
Mtaalamu wa Historia kutoka katika chama cha wanahistoria Tanzania Bw. Jawadu
Mohamed wakati akizungumza na DODOMA FM na kusema kuwa katika karne hii ya 21 kumekuwa na changamoto ya
kutohifadhi kumbukumbu ya mambo yaliyopita yatakayo kuwa na tija kwa kizazi
kijacho.
Bw. Jawadu amesema
katika Jamii ya Watanzania yapo mambo ambayo yamekuwa yakipuuzwa na ni mambo
ambayo nchi zilizoendelea wanayatumia katika kuleta maendeleo kwa mataifa yao
na kwamba ni jambo la hatari kwa Taifa.
Amesema kutokana na
changamoto hiyo taifa linajenga kizazi hewa kisichokuwa na uwezo wa kupambana na
mabadiliko ya mazingira, kushindana na ulimwengu pamoja na kushiondwa kuleta
matokeo chanya katika Taifa.
Sambamba na hayo
amesema katika mambao ambayo yamekosewa katika nchi ni kutokutilia maanani
baadhi ya mambo muhimu ikiwemo makumbusho pamoja na tamaduni na kuona hayana
maana katika jamii.
Na
Phina Nimrod DODOMA FM
Comments
Post a Comment