
Licha ya kutoa
elimu kwa wananchi waishio Swaswa Jijini Dodoma wanaojihusisha na
kilimo kwa kutumia maji taka yanayotajwa kuwa na madhara bado ni changamoto
kwa wananchi hao.
Akizungumza na
Dodoma FM Eng.KASHILIMU MAYUNGA Kutoka Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira
jijini Dododma DUWASA amesema wamefanya jitihada ya kutoa
elimu kwa kufanya vikao mabalimbali lakini wananchi hao wanadai kuwa hawako
tayari kuondoka katika eneo hilo.
Eng.KASHILIMU amesema licha ya kuweka walinzi katika eneo hilo ambao
wanazuia wananchi kuyatumia maji taka hayo bado utekelezaji ni mgumu kwa
wananchi ambao wanasema hawawezi kuondoka na kuacha kwa madai kuwa yanawasaidia katika kilimo.
Kwa upande wake
mkuu wa kitengo cha mawasiliano kutoka mamlaka ya maji safi na usafi wa
mazingira DUWASA Bwana SEBASTIAN WARIOBA amesema mpaka sasa wamechimba mtaro mrefu wa kudhibiti
maji hayo na wamepiga marufuku matumizi ya maji taka kutoka katika mabwawa hayo
na wameongeza walinzi wa suma JKT kwa
ajili ya ulinzi zaidi.
Hata hivyo amebainisha
kuwa kuna mabwawa manne ya maji taka katika eneo la swaswa ambayo ndiyo
wananchi wanayatumia katika kilimo.
Febuary Mwaka huu Naibu Waziri Ofisi
ya Makamu wa Rais Mazingira, Kangi Lugola aliiagiza Mamlaka ya Maji Safi na
Maji Taka Dodoma (DUWASA) kutoa elimu kwa wananchi wanaozunguka maeneo ya
mabwawa yanayohifadhi maji taka kutoyatumia maji hayo kwa kilimo au matumizi
yoyote ya nyumbani.
Lugola alitoa agizo hilo mjini Dodoma alipofanya ziara katika mabwawa yanayohifadhi maji taka yaliyopo maeneo ya Swaswa, ambapo wananchi wa maeneo hayo wameonekana wakiyatumia maji hayo katika kilimo na wengine kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya nyumbani.
Lugola alitoa agizo hilo mjini Dodoma alipofanya ziara katika mabwawa yanayohifadhi maji taka yaliyopo maeneo ya Swaswa, ambapo wananchi wa maeneo hayo wameonekana wakiyatumia maji hayo katika kilimo na wengine kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya nyumbani.
Na,Mindi
Joseph Dodoma FM
Comments
Post a Comment