Katika kuelekea
Dodoma ya kijani walimu wa shule za msingi sekondari na vyuo wameshauriwa
kuanzisha ziara za wanafunzi zinazolenga kutembelea vikundi mbalimbali
vinavyojishughulisha na utunzaji wa mazingira ili kuwapa fursa wanafunzi
kujifunza kuhusu mazingira kwa vitendo.
Ushauri huo unakuja
kufuatia tamko la serikali la kuifanya Dodoma kuwa ya kijani kuonekana kutokuwa
na mwamko mzuri tatizo linalochangiwa na kile kinachosemekana kutokuwa na elimu
ya utunzaji wa mazingira hususani suala la upandaji miti.
Akizungumza na
Dodoma FM Redio kiongozi wa kukundi cha kutunza mazingira CHAPAKAZI kilichopo jijini hapa Bwana DARUWESHI SAIDI amesema
kuwa baadhi ya wananchi jijini hapa wana mwamko wa utunzaji wa mazingira ila
hukwama kutokana na kutokuwa na utaalamu wa kupanda miti hadi kustawi pasppo
kukauka jambo lililopelekea ushauri kutolewa kuwa ni bora elimu hiyo
ikaanzia mashuleni na vyuoni
Katika hatua
nyingine Bwana SAIDI ameiomba serikali
kuhamasisha kwa wingi upandaji miti kwa wananchi kuelekea Dodoma ya kijani kama
ilivyokuwa kwa program zingine ikiwemo ile ya madawati shuleni jambo ambalo
litasaidia jamii kujua hatua za upandaji miti na faida zake
Bwana SAIDI amezitaja faida za upandaji miti
kuwa ni kuleta vimvuli matunda na wakati mwingine huchangia kupatikana mvua kwa
wingi huku akishauri kuanzishwa kwa vikundi vingine vinavyojishughulisha na
utunzaji wa mazingira.
Aidha kiongozi huyo
amewatadharisha baadhi ya watu wanaoharibu mazingira katika kikundi hicho cha
kutunza mazingira CHAPAKAZI kwa
kuvunja miti na kuharibu vibuyu vya kuotesha mimea kwani ni kosa na kwamba
atakayebainika atafikishwa kwenye vyombo vya sheria
Na
RWEIKIZA KATEBALIRWE DODOMA FM
Comments
Post a Comment