Serikali
imesema jumla ya walimu 3655 waliondolewa kazini baada ya kubainika kuwa na
vyeti bandia kufuatia zoezi la uhakiki wa vyeti lililofanywa na serikali katika
kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17 hadi 2017/18.
Naibu Waziri wa
Nchi ofisi ya Rais tawala za Mikoa na Serikali za mitaa TAMISEMI Mh. Joseph
Kakunda ameyasema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma katika mkutano wa Bunge
alipokuwa akijibu swali la Mbunge Nassoro Seleman aliehoji ni wafanyakazi
wangapi waliopoteza ajira zao katika sekta ya elimu kufuatia zoezi hilo.
Naibu Waziri Kakunda amesema katika
zoezi la uhakiki wa vyeti feki Serikali ilidhamiria kubaini watumishi wa umma
walio kuwa na vyeti halali na vyeti vya kugushi zeozi lililofanikisha kubaini
idadi ya walimu 3655 waliokuwa na vyeti vya kugushi.
Amesema baada ya
zoezi hilo yalijitokeza malalamiko pamoja na rufaa mbalimbali kwa watumishi
waliodhani wameonewa na baada ya Serikali kufanya uchambuzi wa kina
iliwarejesha kazini watumishi wapatao 1907 walioondolewa kazini kimakosa huku
akiweka wazi hakuna kiinua mgongo chochote kitakacho tolewa na Serikali kwa
watumishi walio ondolewa kazini wakati
muda wao wa kustaafu ukiwa umekaribia.
Ikiumbukwe kuwa April 28 mwaka 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe
Magufuli akipokea ripoti ya uhakiki wa vyeti feki katika ukumbi wa Chimwaga
hapa Jijini Dodoma aliagiza kuondolewa kazini watumishi zaidi ya 19706 waliobanika
kugushi vyeti ili kujipatia ajira.
Zoezi la uhakiki wa
vyeti kwa watumishi wa umma liliendeshwa na serikali kuanzia mwezi october
mwaka 2016.
Na
Pius Jayunga
Bunge/Dodoma FM
Comments
Post a Comment