
Serikali kupitia ofisi ya
Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISIMI) imewaagiza
wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuhakikisha madarasa ya awali yanakua na
sifa zinazotakiwa.
Naibu waziri wa TAMISEMI Joseph Kakunda amesema kutoka na sera ya elimu ya mwaka 2014 inawataka
wakurugenzi wa halimashauli kutekeleza mambo mabalimbali ya elimu ikiwemo la
uwepo wa madarasa ya awali katika shule zote za msingi.
Aidha amesema katika
kutekeleza sera ya elimu ya mwaka 2014 wakuu wa mikoa,wilaya na wakurugenzi wa
halmashauli wanatakiwa kutimiza wajibu wao na si kusubiri usimamizi kutoka
wizarani .
Naibu Waziri Kakunda amekiri kuwepo kwa uhaba wa walimu maalumu wa darasa la awali na kwamba
wanaendelea kutoa mafunzo kwa walimu ambapo mpaka sasa wametoa mafunzo kwa walimu takribani elf 16.
mpaka mwezi Disemba 2017
shule elfu kumi na sita na nne kati ya shule elfu kumi na sita mia moja na arobani zilikua na darasa la awali ambapo
malengo hadi kufikia mwaka 2020 shule zote za msingi nchini ziwe na darasa la
awali lenye ubora.
Na Mariam Matundu Dodoma FM
Comments
Post a Comment