
Wananchi Mkoani Dodoma wametakiwa kununua dawa kwa ajili ya
kuuwa wadudu vamizi wanaoshambulia mimea katika maduka yanayotambulika na zilizoshahuriwa na wataalamu wa kilimo ili
kuepuka kununua dawa zisizokuwa na ubora na kusababisha hasarara katika mimea.
Ushauri huo umekuja baada ya kuibukua kwa mlipuko wa mdudu
anayejulikana kwa jina la viwaji jeshi anayeshambulia mimea hasa ya mahindi
katika mashamba.
Akizungumza na Dodoma FM Afisa Kilimo wa Mkoa wa Dodoma Bw.
Bernad Abraham amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya wakulima kununua dawa
zilizokwisha muda wake na zilizopoteza ubora na kushindwa kufanya kazi wakati
wa kuipeleka shambani kwa ajili ya matumizi.
Bw. Bernad amesema kila wanapopata taarifa ya kuwepo kwa
wadudu hao wanachukua jitihada ya kutoa elimu kwa wakulima ili kuweza kudhibiti wadudu hao kwa njia
mbalimbali wanazoelekezwa na wataalam wa kilimo .
Akizungumzia athari zilizopatikana Bw. Abraham amesema
hazijaripotiwa athari kubwa kwa Mkoa wa Dodoma lakini yapo maeneo yalioathirika
ikiwemo maeneo ya Dodoma Mjini pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa na
tayari mafunzo yamekwishatolewa kwa wakulima wa maeneo hayo.
Na Phina Nimrod DODOMA FM
Comments
Post a Comment