Halmashauri
ya jiji la Dodoma yawataka wananchi wake kutunza mazingira kwa kufuata taratibu
na maelekezo yaliyotolewa na uongozi wa jiji sambamba na kuwataka wananchi
kuacha kuchimba mchanga kiholela
Hayo
yamebainishwa na mkuu wa idara ya mazingira na udhibiti wa taka ngumu katika
jiji la Dodoma bwana Dickson Kimaro wakati akiongea na kituo hiki ambapo
amewataka watu kufuata maelekezo yaliyotolewa na uongozi wa jiji katika
utunzaji wa mazingira na kwa mtu ambaye ataenda kinyume na taratibu zilizopo atawajibishwa kwa mujibu wa
sheria.
Kwa
upande wake mratibu kanda ya kati NEMC bwna Anord Mapinduzi amewataka wakazi wa
jiji la Dodoma kuunga mkono maamuzi ya Rais wa jamhuri ya muungano w tanzania
Dr john Pombe Magufuli ya kuifanya Dodoma kuwa jiji kwa kuzingatia utunzaji wa
mazingra.
Naye
bwana Kare Limo ambaye ni afisa afya mkoa wa Dodoma amesema mkoa kwa
kushirikiana na uongozi wa jiji wamejiwekea mikakati ya kuimarisha usafi
wa jiji ikiwa ni pamoja na utoaji elimu
kwa wananchi juu ya utunzaji wa mazingira.
Na Victor Makwawa
Dodoma FM
Comments
Post a Comment