Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na changamoto za unyanyasaji na ukatili wa kijinsia kwa waandishi wa habari wanawake hali inayopelekea kutokuwepo kwa wanawake wengi wanaofanya vizuri kwenye tasnia ya habari.
Hayo yameelezwa
na Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Bi,
Edda Sanga wakati akizungumza na dodoma Fm katika kongamano la kilele cha
maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari yaliyofanyika mjini Dodoma.
Bi Eda Sanga
amesema kumekuwepo na baadhi ya viongozi na wamiliki wa vyombo vya habari ambao
wamekuwa wakitumia nafasi zao kwakuwataka kimahusiano watumishi wao kitendo
ambacho kinawadidimiza wanawake na kuwafanya wasifanye vizuri kwenye tasnia ya
habari.
Amesema ukatili
wa kijinsia ikiwemo unyanyasaji katika tasnia ya habari vinaumiza wanawake huku
akiomba mambo hayo yasiendelee ili wanawake waweze kukua kwenye tasnia ya
habari.
Kwa upande wake Mkuu
wa kitengo cha Usuluhishi kutoka TAMWA Bi Gladness Munuo amesema tafiti
zinaonyesha kuwa sauti za wanawake na
vyanzo vya habari za wanawake bado viko chini ikiwa ni pamoja na kutokuwepo kwa
wanawake wamiliki wa vyombo vya habari nchini.
Hata hivyo Katibu wa Jukwaa La Wahariri Tanzania TEF Bwana
Nevile Meena amewataka wanawake waliopo katika tasnia ya habari kupendana na kupeana ushirikiano pale wanawake
wenzao wanapofanya vizuri ama kutaka msaada kutoka kwao huku akitolea mifano
kadhaa kwa wanawake ambao wamekuwa wakikwamisha juhudi za mafanikio ya wanawake
wenzao.
PHINNA NIMRODI Dodoma
FM
Comments
Post a Comment