Skip to main content

VIWANGO VYA MAAMBUKIZI YA UKIMWI TANZANIA NI VIKUBWA


Image result for WAZIRI MKUU





Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kasimu Majaliwa amesema viwango vya maambukizi ya virusi vya ukimwi Nchini bado ni vikubwa kwa mjibu wa utafiti wa nne uliofanyika katika ngazi ya kaya kwa mwaka 2016 hadi mwaka 2017.

Mh. Kasimu Majaliwa ameyasema hayo leo Jijini Dar Es Salaam wakati akizindua mkakati wa maadhimisho ya miaka 15 tangu kuanzishwa kwa mfuko wa dharula wa Rais wa Marekani wa kupambana na kudhibiti maambukizi ya virusi vya ukimwi (PEF)

Amesema watu takribani Mil. 1.4 wanakadiriwa kuishi na virusi vya ukimwi Nchini wengine themanini na moja elfu hupata maambukizi mapya ya virusi vya ukwimi kila mwaka sawa na watu 222,000 kila siku na wahanga wakubwa wa janga hilo wakiwa ni wasichana.

Waziri mkuu ameitaja Mikoa inayoongoza kwa kiwango cha maambukizi makubwa juu ya wastani wa kitaifa wa asilimia 4.7 kuwa mikoa hiyo ni njombe 11.4%, Iringa 11.3%, Mbeya 9.3% Mwanza 7.2% Kagera 6.5% Katavi 5.9%. Shinyanga 5.9% na Dodoma ikiwa 5.0%

Ameitaja Mikoa yenye ongezeko kubwa la watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi kuwa ni pamoja na Mkoa wa Mwanza, Tanga, Kagera, Dodoma, Manyara pamoja na Mkoa wa Iringa na kueleza kuwa takwimu hizo zinalenga kuongeza nguvu zaidi katika kupambana na maambukizi ya virusi vya ukimwi.

Ugonjwa wa ukimwi uligunduliwa Nchini Tanzania mnamo mwaka 1983 na tangu kipindi hicho nguvu kazi kubwa ya Taifa iliendelea kuangamia na kuchangia kupungua kwa kasi ya utoaji wa huduma katika maeneo mbalimbali ikiwemo elimu, afya, kilimo, ufugaji viwanda pamoja na sekta zingine.

Na Pius Jayunga                                                                                  Dodoma FM

Comments

Popular posts from this blog

WAJAWAZITO WASHAURIWA KUTUMIA VIDONGE VYA FOLIC ACID KUEPUKA WATOTO VILEMA

                                                                  Mama wajawazito wameshuriwa kutumia dawa aina ya FOLIC ACID katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito ili kuepuka kupata mtoto mwenye   mapungufu. Rai hiyo imetolewa na Daktari kutoka Hospitali ya Matovyolwa mjini Dodoma   Dk.MUBARACK ISSA ALI wakati akizungumza na Dodoma FM juu ya athari zitokanazo na mama kutotumia dawa hizo. Dr Mubarack amesema katika kipindi cha ujauzito mama huwa anapitia changamoto nyingi hivyo ni vyema akatumia dawa aina ya FOLIC ACID ili kuepuka kupata mtoto mwenye tatizo la mgongo wazi, kichwa kikubwa pamoja na upungufu wa damu. Aidha Dk. Mubarack amesema   ili kuepuka kupata mtoto njiti   kipofu na kusababisha kifo kwa mtoto   ni vyema mama akaepuka matumizi ya pombe, dawa za kulev...

MIKOA INAYOONGOZA KWA UKEKETAJI TANZANIA YATAJWA

Mila potofu   katika jamii ya kimasai imetajwa kuwa changamoto kwa maafisa ustawi wa jamii wa halimashauri ya wilaya ya Ngorongoro  kutokana na kukosa ushirikiano wa kutatua Tatizo la ukeketaji kwa jamii hiyo. Akizungumza na waandishi ya habari Afisa Ustawi Wa jamii Bwana ALOYCE  LOLIKISWALI katika semina iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sanyansi na Utamaduni UNESCO kwa lengo la kupinga ukeketaji wa wanawake amesema kukosekana kwa ushirikiano kwa jamii imekuwa ni changamoto ambayo imepelekea kushindwa kudhibiti ukeketaji pamoja na ukatili wa kijinsia. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Malaigwanan Bwana JOSEPH TIRIPAI amebainisha kuwa mila na desturi zao zitabadilika kulingana na wakati lakini watahakikisha wanalinda watoto wanaozaliwa kutokeketwa na kusisitiza elimu kuendelea kutolewa hususani shuleni. Katika hatua nyingine mratibu wa afya ya mama na mtoto ameeleza kuwa wanawake wajawazito waliokeketwa wanalazimika   kujifug...

MITI YA KIVULI MAARUFU KAMA PANGA UZAZI YAZUA TAHARUKI WILAYANI BAHI DODOMA

                                                  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bahi Jijini Dodoma Dk.Philipina Philipo amewatoa hofu wakazi   wa Wilaya hiyo juu ya taarifa za kuwepo kwa madhara katika miti ya kivuli maarufu kama PANGA UZAZI ambayo imezua hofu kwa wananchi hao. Hoja hiyo imeibuliwa katika kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo ambapo baadhi ya madiwani wameomba kupatiwa ufafanuzi kuhusu kuwepo kwa fununu kuwa mti huo una madhara na kuongeza kuwa baadhi ya wananchi wameanza kuikata wakihofia kupatwa na madhara hayo. Akitoa ufafanuzi kuhusu miti hiyo Mganga Mkuu wa Wilaya Dk.Philipina Philipo amesema hadi hivi sasa hakuna utafiti wowote uliofanyika na kubainisha kuwa mti huo hauna madhara hivyo wananchi hawana haja ya kuhofia chochote. Kutokana na Majibu hayo ya DK PHILIPINA yamepelekea kuibua kwa hoja nyingine kwa madi...