Upungufu wa walimu
wa somo la hisabati katika shule za sekondari umechangia kwa kiasi kikubwa
wanafunzi kutofanya vizuri somo hilo huku wengi wao wakiacha kabisa kulisoma na kujikita zaidi katika masomo ya sanaa.
Wakizungumza na
kituo hiki baadhi ya wanafunzi wamekiri kuwepo kwa walimu wachache wa somo hilo
pamoja na walimu kuwa wakali kitu
ambacho kinapelekea wengi wao kushindwa kabisa kusoma somo hilo huku pia wakikatishwa tamaa na wanafunzi waliowatangulia kwa kusema somo hilo ni ngumu.
Mwalimu SOPHIA MDEI ambaye ni mwalimu wa somo la hisabati amesema
changamoto kubwa inayowakabili ni kuwepo kwa walimu wachache hali ambayo
imepelekea kuwa na vipindi vingi na kusababisha kushindwa kumfuatilia
mwanafunzi mmoja mmoja.
Aidha kwa upande
wake afisa elimu sekondari Halimashauri ya jiji la Dodoma Mwalimu ABDALLAH MEMBE
amesema kutokana na changamoto hiyo serikali tayari imeweka mkakati wa
kuhakikisha somo hilo linafanya vizuri katika shule zote nchini ikiwa ni kuongeza walimu kwa lengo
la kuimarisha ufaulu wa somo hilo.
Mwalimu MEMBE ameongeza
kuwa Ili kuberesha ufaulu wa somo hilo wanafunzi wametakiwa kuacha kukata tamaa
kwa kusema somo hilo ni gumu badala yake kuweka jitihada nyingi kama wanavyofanya katika masomo
mengine.
Na,Mindi
Joseph Dodoma
FM
Comments
Post a Comment