
Wadau wa kupinga
vitendo vya ukeketaji wametoa maoni yao kwa kuitaka serikali kuanzisha mitaala
ya somo la kupinga ukeketaji kuanzia shule za msingi na sekondari Nchini.
Wametoa maoni Hayo
wakati wa warsha ya kupinga vitendo vya ukeketaji inayoendelea katika tarafa ya
Loliondo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Akizungumza na
Dodoma Fm Mwenyekiti wa Malaigwanani Bwana Joseph Tripai wakati akiwasilisha
Mada juu ya kutokomeza vitendo vya ukeketaji ameitaka serikali kupitia Wizara
ya elimu kuanzisha mtaala wa somo hilo ili kuanza kutoa elimu y'a kupinga
vitendo hivyo kuanzia kwa watoto wa shule wangali wadogo.
Kwa upande wake
Afisa wa polisi wa dawati la jinsia Wilayani Ngorongoro Remmiguis Williams
amebainisha Changamoto kadhaa ikiwemo usiri kutoka kwa wazazi, ndugu Na jamii
kwa ujumla zimekua zikirudisha nyuma jitihada za kutokomeza vitendo vya
ukeketaji.
Ameongeza kuwa
baadhi wanajua vitendo vya ukeketaji ni kosa kisheria hivyo huogopa kutoa
taarifa kwa jeshi la polisi kwa kuhofia ndugu zao kupelekwa mahakamani na
kufungwa.
Warsha hii
inaendelea wilayani Ngorongoro katika tarafa ya Loliondo kwa kushirikiana Na shirika
la Umoja wa Mataifa elimu sayansi Na utamaduni UNESCO ambapo imewakutanisha
baadhi ya Waandishi kutoka katika Mikoa mitano inayoongoza kwa vitendo vya
ukeketaji ikiwemo, Manyara, Dodoma, Mara, Arusha na Singida.
Na Lucas Godwin Chanzo:Dodoma FM
Comments
Post a Comment