
Wazazi wameshauriwa kuzingatia kutoa malezi
bora kwa watoto ndani ya familia na jamii kwa ujumla ili kuwa na taifa lenye
uchu wa kujiletea maendeleo.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu
wa Wilaya ya Kondoa Mhe.Vaileth Makota wakati akisoma Hotuba ya
waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika
maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani yaliyofanyika Wilayani Kondoa jijini
Dodoma .
Mhe. Vaileth Makota
amesema wazazi wana wajibu wa kuwalea watoto katika malezi bora na katika
maadili mazuri ili kujenga taifa bora lenye watoto wanaojitambua,
wanaojithamini, na wenye maadili mema ili kulitumikia Taifa.
Ameongeza kuwa wazazi
wanatakiwa kuwa walimu kwa matendo yao kwa watoto kwani watoto wanaiga yale
ambayo wazazi wanafanya hivyo tabia na mienendo yao ni kati ya vitu ambavyo
vitasababisha malezi mabaya au bora kwa watoto na jamii kwa ujumla.
Amesisitiza kuwa
wazazi wana wajibu wa kuwalea watoto katika malezi bora ili kujenga utu,
uzalendo na upendo kwa watoto na jamii kwani malezi katika familia ni msingi
katika ujenzi wa taifa linalozingatia uzalendo, maadili mema, utu na
uwajibikaji katika maendeleo yao na taifa.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mtoto nchini Tanzania Bibi. Magreth Mussai amesisitiza watoto
na vijana kuwa na maadili kwa wazazi na wanajamii ili kujenga taifa lenye
maadili na upendo.
Siku ya Familia
Duniani inaadhimishwa kila Mei 15, 2018 na kwa mwaka huu imeadhimishwa ikienda
na kaulimbiu isemayo “Malezi Jumuishi: Msingi wa Uzalendo, Utu na Maadili ya
Familia na Taifa’’.
Mariam
Matundu
DODOMA FM
Comments
Post a Comment