
Wananchi wa Jiji la Dodoma wameaswa kuacha uharibifu wa misitu
ambao umechangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa
jangwa na atakayebainika hatua
kali za kisheria zitachuliwa dhidi yake kutokana na kuchangia uchafuzi wa mazingira.
Rai hiyo imetolewa leo na Afisa Misitu wa Halmashauri ya
jiji la Dodoma ALEXANDER KABADO wakati
akizungumza na Dodoma FM juu ya tathmini ya uharibifu wa Mazingira.
Bwana Kabado amesema wanakabiliwa na wimbi kubwa la uharibifu wa misitu unaotokana
na kilimo cha kuhama hama ambapo asilimia kubwa wanajihusisha na kilimo pamoja
na uchomaji wa mkaa.
Ameeleza kuwa katika kukabiliana na changamoto hizo wameweka
mikakati ya kuhifadhi na kuzuia uharibifu katika maeneo ya misitu na kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa utunzaji
misitu pamoja na kuwahimiza wananchi kupanda miti katika mashamba yao.
Kwa upande wao baadhi ya wanachi wamekiri kuwepo kwa
uharibifu wa misitu kutokana na matumizi ya nishati ya mkaa hali ambayo
imepelekea kuwepo kwa ukame licha ya kuwepo zoezi la upandaji wa miti lakini
changamoto kubwa ni ukosefu wa mvua zitakazopelekea kukua kwa miti hiyo.
katika maadhimisho ya siku ya
wafanyakazi ambayo yalifanyika jana jijini Dodoma katika risala ya mgeni rasmi changamoto kubwa iliyobainishwa
na mjumbe wa kamati ya utendaji TUICO mkoa
kwa niaba ya wafanyakazi GODFREY
NDOSHI,alibainisha mkoa wa Dodoma
bado unakabiliwa na ukame pamoja na jangwa kutokana na uharibifu wa misitu.
Na,Mindi Joseph Chanzo
Dodoma FM
Comments
Post a Comment