Kutokana
na Athari za mabadiliko ya tabia nchi katika mfumo wa
Ki-ekolojia na Usalama wa Chakula Mashariki mwa Afrika, jamii imetakiwa
kuchukua hatua thabiti kukabiliana na mabadiliko hayo.
Mkoa wa Dodoma unatajwa kupoteza mahindi ambayo
inagharimu kiasi kikubwa cha fedha kila mwaka kutokana na
wadudu waharibifu.
Hayo yamebainisha katika Kata ya Hombolo
Bwawani Jijini Dodoma na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA)
wakati wa kutoa elimu kuhusu kilimo kwa kutumia shamba darasa.
Kwa mujibu wa muwakilishi wa shirika hilo Dk.
Fredy amesema kuwa, elimu hiyo ya shamba darasa kwa wakulima
ni kipimo kwa Utafiti wa wadudu wanaoharibu mazao na unalenga katika
kupata suluhu ya kukabiliana na magonjwa ya mahindi, akiwemo funza ambaye
amekuwa ni mharibifu katika zao la mahindi, katika ukanda wa
kati.
Pamoja na hayo mtaalamu huyo amesema kuwa IITA imejipanga kuwajengea
uwezo wakulima hao kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kutumia
tekinolojia muhimu katika ikiwemo kuanzisha mashamba yanayoonyesha kilimo cha
kukabiliana na mabadiliko hayo.
Kutokana na hayo mhifadhi wa udongo na uvunaji wa maji ya mvua
shambani kutoka taasisi ya utafiti Hombolo Bw.Elirehema Swai aliishauri taasisi
ya IITA kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa wakulima nchini kuhusu kadhia ya Sumu
Kuvu kwa mazao ya chakula.
Kwa upande wake muwakilishi wa katibu mkuu wizara ya kilimo
Bi.Shakwanende Natai aliwataka wakulima wa kata ya Hombolo kutumia mbegu bora
ili kuepusha magonjwa kwa mimea kwa kuzingatia utaalamu wa kisasa.
Naye Afisa kilimo wa Halmashauri wa jiji George Mhina
aliwaambia wakulima wa kata ya Hombolo kuchukua jukumu la kukagua mazao mara
kwa mara na pindi wanapoona mabadiliko yasiyo ya kawaida watoe taarifa mapema
kwa wataalamu wa kilimo .
Mbali na hayo amesema,ili wakulima hao wapate mazao
yanayostahili wanapaswa kuzalisha kisasa kwa kuwatumia wataalam wa kilimo ikiwa
ni pamoja na kuzingatia mazao yanayostahili ukame.
Na ANIPHA
RAMADHAN CHANZO:DODOMA FM
Comments
Post a Comment