Kutokana na
kuwepo kwa changamoto za ajira Nchini imebainishwa kuwa asilimia kubwa ya Wanawake Jijini Dodoma wamejiunga na ufugaji
wa nyuki wa kisasa katika hifadhi za misitu kwa lengo la kujipatia
kipato pamoja na kuokoa uharibifu wa hekta 7,270 wa misitu Nchini Tanzania.
Wakizungumza na Dodoma fm baadhi ya wanawake wamesema
ufugaji wa nyuki una umuhimu mkubwa kwani unasidia kuboresha mazingira na
kuondokana na uharibifu wa mazingira.
Katika hatua nyingine Wamebainisha kuwa Ufugaji wa nyuki katika maeneo mengi ya
Tanzania unafanyika kuzalisha kipato, lakini pia ufugaji huo una madhumuni makuu mawili ya kuingiza
kipato na kuimmarisha mazingira.
Kwa upande wake afisa misitu wa halimashauri ya jiji la
Dodoma BW,ALEXENDAR KABADO amebainisha kuwepo kwa idadi kubwa ya wanawake ambao
wameonyesha ushirikiano kwa kujiunga katika vikundi vya ufungaji wa nyuki na imechangia
kwa kiasi kuondoa uharibifu wa hifadhi.
Aidha bw,KABADO ameongeza kuwa katika kata 41 za
halimashauri ya jiji la Dodoma kuna vikundi
zaidi ya 30 vya ufugaji wa nyuki huku wanawake wakiongoza kwa kuweka kipaumbele
zaidi.
Na,Mindi
Joseph Dodoma
FM
Comments
Post a Comment