Kufuatia
tamko la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli
kuitangaza Dodoma kuwa Jiji, Waziri mkuu Kasimu Majaliwa amesema tayari
taratibu za kulitambua Jiji la Dodoma kisheria zimeshaanza kufanyika.
Waziri
Mkuu Kasimu Majaliwa ameyasema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma katika kipindi
cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri mkuu wakati akijibu swali la Mbunge wa
kuteuliwa Felista Aloyce Bula aliehoji ni lini Serikali italeta mswada wa
sheria wa kuitambua Dodoma kama Jiji.
Amesema
kama ambavyo Mh. Rais ana mamlaka ya kutangaza eneo lolote kulipa hadhi ya Jji,
hivyo Serikali kupitia vyombo vyake huanza taratibu za kuingiza maelekezo hayo
kisheria na tayari wanasheria, Tamisem, ofisi ya Waziri mkuu wameanza kufanyia
kazi swala hilo ili litambulike rasmi kisheria.
Waziri
mkuu amesema kisheria Rais ana mamlaka ya kupandisha hadhi mji wowote iwapo
umekidhi vigezo muhimu ikiwemo huduma ya maji, afya, miundombinu ya barabara
sambamba na kuimarika kwa zoezi la ukusanyaji wa mapato vigezo ambavyo Jiji la
Dodoma limekidhi.
Waziri
Mkuu amewataka wakazi wa Dodoma kutumia fursa hiyo kama sehemu ya wao
kujiongezea kipato kupitia shughuli mbalimbali kutokana na Dodoma kukua ikienda
sambamba na ongezeko la mahitaji muhimu ikiwemo chakula kwa wakazi wa Jiji la Dodoma.
Na Pius Jayunga Dodoma
FM
Comments
Post a Comment