
Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini
(SUMATRA) jijini Dodoma kwa kushirikiana
na jeshi la polisi imetoa tahadhari kwa waendasha
bodaboda kutobeba watoto wenye umri chini ya miaka 9.
Akizungumza na DODOMA FM mapema leo Afisa mfawidhi wa
SUMATRA Bwana Konradi Shio amesema sheria hairuhusu kubeba mtoto peke yake kwenye
pikipiki za magurudumu mawili licha ya kuwepo kwa madai ya bodaboda kuwa
wanajipatia kipato.
Bwana Shio ameongeza kuwa kwa mujibu wa sheria wanawachukulia
hatua kali bodaboda kwa kuwatoza faini, na kuwapeleka jela lakini bado kuna upuuzwaji
wa sheria hiyo hivyo wamekuwa wakipendekeza kuwapeleka mahakamani ili kupewa
fundisho.
Katika Hatua nyingine amebainisha madhara ya kubeba mtoto
chini ya umri wa miaka 9 kwenye bodaboda na tayari wameanzisha operationi
ambayo inafanywa na jeshi la polisi muda wa asubuhi watoto wanapoenda shule pamoja
na jioni wanaporudi kutoka shule ili kuhakikisha bodaboda hao wanawakamata na kuwafikisha
katika vyombo vya sheria.
Ili kuondokana na changamoto hii waendesha bodaboda wametakiwa kuacha kuwabeba
watoto hao chini ya umri wa miaka 9 ikiwa
ni pamoja na kuzingatia sheria za barabarani.
Na,Mindi Joseph Dodoma
FM
Comments
Post a Comment