Imeelezwa kuwa wanahabari
wana jukumu la kuhakikisha wanaijenga jamii na kuifanya huwa imara kwa
kuwafikishia taarifa za usahihi pamoja na kufichua matukio ya uhalifu
ikiwemo dawa za kulevya.
Hayo yameelezwa na Spika
wa bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai katika kongamano la
maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani ambayo kitaifa
yamefanyika hapa Jijini Dodoma.
Spika Ndugai amesema kuwa
kumekuwa na changamoto ya baadhi ya watu kusambaza matukio ya uongo katika
Mitandao mbalimbali ya kijamii hali inayopelekea usumbufu na sintofahamu kwa
jamii.
Nae Makamu wa Rais wa
Klabu za Waandishi wa habari Tanzania Bi.Jane Mihanje amesema katika
kuhakikisha wanahabari wanatumia kalamu na karatasi kwa ajili ya maslahi ya
wananchi wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya wanahabari kukutana na matukio ya
kutekwa pamoja na kuuawa.
Aidha Bi Jane amesema kuwa
wanahabari wanahofia kufanya kazi kwa Uhuru kutokana na vitisho wanavyokutana
navyo hivyo Serikali ikemee na kuvipinga vitendo hivyo.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Mashindano ya Ulimbwende nchini Tanzania Bi. Salome Kitari
ameiomba Serikali kukemea matukio yanayofanywa juu ya wanahabari hususani ya
kutekwa .
Maadhimisho ya siku ya
Uhuru wa vyombo Vya Habari Mwaka 2018 yamebebwa na Kauli Mbiu isemayo wajibu wa
sheria, vyombo vya habari, haki na sheria.
Na Phinna Nimrodi Dodoma
FM
Comments
Post a Comment