
Shirikisho la watu
wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) limeombwa kuitisha na kufanya vikao vya
mara kwa mara ili kujadili mambo mbalimbali yanayohusiana na walemavu.
Rai hiyo imetolewa na Mjumbe wa kamati ya watu wenye ulemavu mkoa
wa Dodoma ambaye pia ni fundi mkuu katika karakana ya kutengeneza vifaa visaidizi kwa watu wenye ulemavu wa viungo jijini Dodoma (KAWADO) Bwana MWITA MARWA wakati akizungumza na Dodoma FM.
Bwana Marwa amesema shirikisho hilo litakapoweka utaratibu wa kukutana mara kwa mara
itasaidia watu wenye ulemavu kuweka mipango itakayowasaidia ikiwa ni pamoja na kujadili namna ya kupata
ufadhili jambo ambalo litawasaidia kujikwamua kiuchumi.
Amesema kutofanya
vikao kwa washirika katika shirikisho hilo kunapelekea kila mmoja kuanzisha
mradi wake binafsi jambo ambalo linapelekea baadhi yao kukwama kutokana na
uwezo wa mitaji huku akisema changamoto hizo zinaweza kupungua kama watakuwa na
utaratibu wa kukaa kwa pamoja na
kujadili.
Fundi huyo mkuu wa
(KOWADO) amesema kwa kuzitambua changamoto za walemavu wa viungo jijini Dodoma karakana hiyo ilianza
kutengeneza vifaa visaidizi mbalimbali kwa ajili ya walemavu wa viungo kama
baiskeli na kuingia tenda za kutengeneza vifaa hivyo kwa watu nje na walemavu
na hata serikalini japo amesema changamoto kubwa ikiwa ni uwezeshwaji.
Hata hivyo ameiomba
serikali kuwapa kipaumbele walemavu kwa kuwawezesha katika shughuli
wanazozifanya kingine ikiwa ni kuwatengenezea mazingira ya kufika sehemu husika
kwa urahisi mfano baadhi ya ofisi zilizokojuu zimekuwa hazina lifti jambo
ambalo ni changamoto kwao.
Na
RWEIKIZA KATEBALIRWE DODOMA FM
Comments
Post a Comment