
Wananchi
wilayani kongwa wametakiwa kutumia mafunzo wanayopatiwa na mashirika mbalimbali
yasiyo ya kiserikali kuleta maendeleo kwa kutambua matumizi sahihi ya mpango wa
matumizi ya aridhi pamoja na kuhakikisha wanatatua migogoro sugu ya ardhi
katika maeneo yao.
Wito
huo umetolewa leo na Diwani wa kata ya kongwa Bwana White Zubery wakati akifungua
mdahalo wa haki za ardhi wilayani kongwa wenye lengo la kutambua usimamizi wa
mpango wa matumizi sahihi ya ardhi na uundwaji wa vyombo vya utatuzi wa migogoro
ya ardhi vijijini unaotekelezwa na shirika la PELUM TANZANIA katika
wilaya za Kongwa na Bahi Jijini Dodoma.
Amesema
kuwa ni vyema wananchi wakatumia mafunzo hayo kwani awali katika vijiji kama
vya Lenjulu , chilangilizi ,Iduo na Suguta kulikuwa na migogoro mingi
inayohusisha wakulima na wafugaji ambapo kupitia mafunzo yanayotolewa na
shirika la PELUM TANZANIA maeneo mengi migogoro hiyo imetatuliwa.
Aidha
amewataka kutumia mafunzo hayo kwa manufaa ya wananchi wengine walioko katika
maeneo mbalimbali ya nje na wilaya hiyo na kuacha kuitegemea serikali ifanye
kila jambo.
Awali
akitoa taarifa fupi mbele ya mgeni rasimi afisa mradi kutoka shirika la PELUM
TANZANIA Bi Anna Marwa Amesema kuwa wameamua kutoa mafunzo
hayo kwa lengo la kuwajengea viongozi na wananchi uelewa mkubwa ili kutambua
sheria mbalimbali zinazohusu masuala ya ardhi ambapo amedai baada ya mafunzo
hayo kutolewa migogoro ya ardhi imepungua kwa asilimia 70 katika wilaya ya
Kongwa.
Nao
baadhi ya wananchi walioshiriki katika mdahalo huo wamelipongeza shirika hilo
kwa kutoa mafunzo hayo kwani mradi huo umewasaidia kutambua sheria
mbalimbali ambazo zimekuwa zikiwasaidia katika kutatua migogoro ya ardhi pamoja
na ile ya wakulima na wafugaji.
Shirika
la PELUM TANZANIA lenye makao makuu yake mkoani Morogoro
linatekeleza mradi wa ushiriki wa wananchi katika kusimamia sekta ya kilimo na
unatekelezwa katika mikoa mitatu na wilaya sita ambayo ni Morogoro ,Iringa na
Dodoma ambapo katika mkoa wa Dodoma unatekelezwa katika wilaya ya bahi na
Kongwa ndani ya vijiji 30.
Na Alferd Bulahya Dodoma FM
Comments
Post a Comment