
Waganga wa tiba za
asili wameshauriwa kuwa wakweli juu ya magonjwa wanayotibu pale wagonjwa
wanapohitaji tiba kutoka kwao huku serikali ikiombwa kuwa bega kwa bega na
sekta ya tiba za asili ili kutatua changamoto zinazoikabili.
Ushauri huo unakuja
baada ya kuwepo kwa kile kinachosemekana kuwa wapo waganga wa kienyeji ambao hujivisha
kofia za kutibu magonjwa yote jambo linalosemekana wao ndiyo chanzo cha mauaji
ya watu wenye ualbino.
Akizungumza na
Dodoma FM kupitia kipindi cha Dodoma Live katibu wa umoja wa waganga na wakunga
tiba asili Tanzania (UWAWATA) Bwana LUCAS
MLIPU amesema kuwa wapo waganga ambao taaluma zao sio za kiuweledi jambo
ambalo uwafanya kutoa tiba za uongo na kwa masharti mazito yanayopelekea
kuharibu sifa za waganga wa asili huku akiomba serikali kushirikiana na waganga
wa tiba asili kuwabaini wakweli na waongo.
Bwana MLIPU ameiomba serikali itambue mchango
wa uwepo wa msemaji mkuu wa tiba asili ambaye atasaidia kuelezea uwezo wa waganga
hao na matabaka yao.
Naye mkurugenzi wa Taasisi
ya Hope Derivery Foundation inayoshirikiana na wadau mbalimbali kudhibiti
ukatili kwa watu wenye ualbino Bwana MAIKO
SALALI amesema ni veyma waganga hao
wakajitathimini na kutoa majibu juu ya
tuhuma zinazowaandama na kuwahakikishia usalama watu wenye ualbino kwa
kutowadhuru huku akisema hata wachimba madini na wafanyabiashara wanahusishwa
katika vitendo hiyo kutokana na imani zao.
Na
RWEIKIZA KATEBALIRWE DODOMA
FM
Comments
Post a Comment