Skip to main content

SERIKALI YAKUTANA NA WADAU KUJADILI UTEKELEZAJI WA MIPANGO YA UKATILI WA KIJINSI







Serikali imekutana na wadau wa Maendeleo Jijini Dar es Salaam kujadiliana kuhusu utekelezaji wa Sera na Mipango ya kitaifa inayohusu masuala ya jinsia ikiwemo Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza vitendo  vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto  (2017/18 – 2021/22).
utekelezaji wa mikataba ya kikanda na kimataifa kuhusu kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa Wanawake kiuchumi. 

Akizungumza katika kikao kati ya Serikali na wadau hao Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Sihaba Nkinga amesema Serikali imeamua kukutana na wadau ili kujadiliana na kupata maoni kuhusu utekelezaji wa Sera Mipango na mikakati ya Serikali katika masuala ya kijinsia ili kuweza kutekeleza kwa mafanikio masuala hayo.

Ameongeza kuwa Serikali inashirikiana na wadau wa Maendeleo kwa karibu ili kuwa na Mipango na  mikakati ya pamoja ya kutekeleza masuala mbalimbali ya kijinsia ikiwemo kutokomeza vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto na uwezeshaji wa Wanawake kiuchumi.

"Ni jambo la busara kuwashirikisha wadau wa Maendeleo katika masuala ya kimaendeleo ili kupeleke mbele kurudumu la maendeleo" alisisitiza Bi. Sihaba.
Akizungumzia utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza vitendo vya  Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto  (2017/18 – 2021/22)(NPA) Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sera na Mipango kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Atupele Mwambene amesema kuwa Serikali imetekeleza Mipango huo kwa mafanikio tangu kuzinduliwa kwake na  masuala mbalimbali yametekelezwa katika Mipango huo ikiwemo kuwawezesha maafisa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii kutoa elimu juu ya vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto iliyosaidia kupunguza vitendo hivyo hasa katika maeneo ya vijijini.

Kwa upande wake Muwakilishi wa UN Women nchini  Bi. Susan Steffen akizungumza kwa niaba ya wadau wa Maendeleo ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwashirikisha katika masuala mbalimbali ya Maendeleo na kuahidi kuendelea kushirikiana katika masuala mbalimbali kwa manufaa ya taifa la Tanzania.

Na Mariam Matundu                                               DODOMA FM

Comments

Popular posts from this blog

WAJAWAZITO WASHAURIWA KUTUMIA VIDONGE VYA FOLIC ACID KUEPUKA WATOTO VILEMA

                                                                  Mama wajawazito wameshuriwa kutumia dawa aina ya FOLIC ACID katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito ili kuepuka kupata mtoto mwenye   mapungufu. Rai hiyo imetolewa na Daktari kutoka Hospitali ya Matovyolwa mjini Dodoma   Dk.MUBARACK ISSA ALI wakati akizungumza na Dodoma FM juu ya athari zitokanazo na mama kutotumia dawa hizo. Dr Mubarack amesema katika kipindi cha ujauzito mama huwa anapitia changamoto nyingi hivyo ni vyema akatumia dawa aina ya FOLIC ACID ili kuepuka kupata mtoto mwenye tatizo la mgongo wazi, kichwa kikubwa pamoja na upungufu wa damu. Aidha Dk. Mubarack amesema   ili kuepuka kupata mtoto njiti   kipofu na kusababisha kifo kwa mtoto   ni vyema mama akaepuka matumizi ya pombe, dawa za kulev...

MIKOA INAYOONGOZA KWA UKEKETAJI TANZANIA YATAJWA

Mila potofu   katika jamii ya kimasai imetajwa kuwa changamoto kwa maafisa ustawi wa jamii wa halimashauri ya wilaya ya Ngorongoro  kutokana na kukosa ushirikiano wa kutatua Tatizo la ukeketaji kwa jamii hiyo. Akizungumza na waandishi ya habari Afisa Ustawi Wa jamii Bwana ALOYCE  LOLIKISWALI katika semina iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sanyansi na Utamaduni UNESCO kwa lengo la kupinga ukeketaji wa wanawake amesema kukosekana kwa ushirikiano kwa jamii imekuwa ni changamoto ambayo imepelekea kushindwa kudhibiti ukeketaji pamoja na ukatili wa kijinsia. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Malaigwanan Bwana JOSEPH TIRIPAI amebainisha kuwa mila na desturi zao zitabadilika kulingana na wakati lakini watahakikisha wanalinda watoto wanaozaliwa kutokeketwa na kusisitiza elimu kuendelea kutolewa hususani shuleni. Katika hatua nyingine mratibu wa afya ya mama na mtoto ameeleza kuwa wanawake wajawazito waliokeketwa wanalazimika   kujifug...

MITI YA KIVULI MAARUFU KAMA PANGA UZAZI YAZUA TAHARUKI WILAYANI BAHI DODOMA

                                                  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bahi Jijini Dodoma Dk.Philipina Philipo amewatoa hofu wakazi   wa Wilaya hiyo juu ya taarifa za kuwepo kwa madhara katika miti ya kivuli maarufu kama PANGA UZAZI ambayo imezua hofu kwa wananchi hao. Hoja hiyo imeibuliwa katika kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo ambapo baadhi ya madiwani wameomba kupatiwa ufafanuzi kuhusu kuwepo kwa fununu kuwa mti huo una madhara na kuongeza kuwa baadhi ya wananchi wameanza kuikata wakihofia kupatwa na madhara hayo. Akitoa ufafanuzi kuhusu miti hiyo Mganga Mkuu wa Wilaya Dk.Philipina Philipo amesema hadi hivi sasa hakuna utafiti wowote uliofanyika na kubainisha kuwa mti huo hauna madhara hivyo wananchi hawana haja ya kuhofia chochote. Kutokana na Majibu hayo ya DK PHILIPINA yamepelekea kuibua kwa hoja nyingine kwa madi...