Serikali
imesema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2014/15 iltoa ruzuku ya pembejeo za
kilimo kupitia vikundi vya wakulima pamoja na Bank jamii badala ya utaratibu wa
vocha za pembejeo zilizokuwa zikitumika hapo awali.
Naibu
Waziri wa kilimo Dr. Merry Mwanjelwa ameyabainisha hayo Bungeni Jijini Dodoma
wakati akijibu swali la Mbunge Jackline Ngonyani aliehoji ni lini Serikali
itawalipa mawakala wa kilimo ambao waliikopesha Serikali tangu mwaka 2014/15.
Amesema
utaratibu huo ulitumika ili kuwajengea uwezo wa kulima kuto kukopa na kujipatia
pembejeo wao wenyewe na Serikali ilitakiwa kuchangia 20% ya gharana za pembejeo
kwa hekali moja utaratibu uliopangwa kutumika Nchi nzima lakini Mikoa Morogoro,
Njombe, Iringa Manyara, Mbeya Ruvuma Rukwa na Tabora ndio iliyotekeleza agizo
hilo
Naibu
waziri huyo amesema uhakiki wa awali ulifanyika katika Mikoa ipatayo kumi, na
kupitia uhakiki huo imejiridhisha kuwepo kwa mapungufu katika baadhi ya
makampuni na mawakala ikiwemo kukosekana kwa nyaraka za manunuzi, kuto kuwepo
kwa mikataba ya kazi, kukosekana kwa orodha ya wakulima wanufaika katika vijiji
husika.
Ameongeza
kuwa Serikali itaboresha sekta ya kilimo Nchini kupitia malipo kwa mawakala na
uhakiki ukiwa bado unaendelea baada ya kukamilika taarifa rasmi itatolewa ili
kukamilisha malipo hayo..
Na Pius Jayunga Bunge/Dodoma FM
Comments
Post a Comment