Serikali imekiri
kuwepo kwa changamoto ya miundombinu ya mambweni kwa shule za sekondari
kutokana na ongezeko la wanafunzi kufuatia mpango wa elimu bila malipo.
Naibu waziri wa
elimu sayansi na teknolojia mh Willium Tate Ole Nasha amebainisha hayo wakati akizungumza
na Dodoma FM juu ya tahtmini ya hali ya miundombinu mbinu katika shule za
sekondari.
Mh.Ole Nasha
amesema kuwa serikali inatambua changamoto hiyo na kwamba kupitia bajeti ya
mwaka wa fedha 2018/2019 wizara imedhamiria kuendelea kutatua changamoto hiyo.
Amesema serikali
imekuwa ikiendesha mpango wa lipa kulingana na matokeo ambao umesaidia kutatua
changamoto ya miundombinu katika shule nyingi nchini ambapo kwa kipindi cha
miaka 2 jumla ya mabweni 338 yamejengwa nchi nzima.
Katika hatua
nyingine Naibu waziri Ole Nasha amewataka wazazi na walimu kuendelea kutoa
nasaha kwa wanafunzi hususani wa kike ili kujiepusha na vishawishi
vitakavyopelekea kukatisha masomo wakati serikali ikiendelea kutatua changamoto
ya mabweni.
Kwa mwaka wa fedha
2018/2019 serikali imetenga bilioni 140 zilizoelekezwa katika wizara ya elimu.
Mariam
Matundu Chanzo:Dodoma
FM
Comments
Post a Comment