Serikali kupitia
ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge Kazi Ajira na watu wenye ulemavu imeandaa muogozo
wa kitaifa wa mafunzo ya vitendo kwa wahitimu wa elimu ya juu pamoja na vyuo
vya ufundi ili kusaidia wadau kuandaa, kusimamia, pamoja na kuratibu mafunzo ya uzoefu kazini kwa
wahitimu.
Hayo yamebainishwa leo
Bungeni Jijijini Dodoma na Naibu Waziri
ofisi ya Waziri Mkuu Mh. Anthony Mavunde wakati akijibu swali la Mbunge wa viti
maalumu Zainabu Athumani Katimba
aliehoji Serikali haioni haja ya kutungwa kwa sera ya mafunzo kwa
vitendo kazini kwa wahitimu wa elimu ya juu na vyuo vya ufundi ili vijana
waweze kupata ujuzi utakaoendana na soko la ajira.
Akijibu swali hilo Mavunde amesema Serikali
imeona kuna haja ya kuandaa miongozo ya kitaifa ya kisera ya mafunzo kwa
vitendo kwa wahitimu wa ngazi mbalimbali mwongozo uliozinduliwa mwezi septemba
mwaka 2017 na kuanza kutumika rasmi katika mwaka wa fedha 2017/18 ambapo zaidi
ya nafasi 750 zimetolewa na waajiri pamoja na kufanya mafunzo kwa vitendo.
Aidha Mavunde amesema baada ya
kupitishwa kwa sera hiyo swala la mafunzo kwa vitendo kwa wahitimu litawekwa
katika sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 na kupitia mkutano huo
Mh. Mavunde ametoa wito kwa wa ajiri Nchini kushirikiana na Serikali katika
utekelezaji wa mpango wa mafunzo kazini katika maeneo yao ya kazi.
Kwa upande wake
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri mkuu sera, bunge, kazi, ajira na wenye ulemavu
Mh. Jenister Mhagama amesema kazi kubwa ya ofisi ya Waziri mkuu ni kuungana na
wadau wa Wizara ya elumu kupitia vyuo vikuu Nchini ili kuwaandaa vijana
wahitimu wa elimu ya juu kuingia katika soko la ajira.
Katika mkutano huo
jumla ya maswali kumi yameulizwa na Waheshimiwa. Wabunge na kisha kutolewa
majibu kupitia wizara husika.
Na
Pius Jayunga DODOMA FM
Comments
Post a Comment