Serikali imeanza mchakato wa kuwasaidiwa wafanyabiashara wa kata ya Tambuka reli Jijini Dodoma kwa kuwapatia soko la kudumu.
Akiongea na Dodoma FM juu ya utatuzi wa changamoto hiyo Diwani wa kata hiyo Bwana
Juma Mazengo amesema changamoto hiyo imekuwa ikiwakabili wananchi hao kwa muda
mrefu, na kwa sasa serikali imeanza kuitatua iyo.
Aidha Bwana Mazengo
amesema, ujenzi wa soko hilo ukikamilika utafungua fursa za kimaendeleo kwa
wakazi wa eneo, na kuwataka wananchi kutunza miundombinu iliyopo katika maeneo
yao sambamba na kushiriki katika shughuli za kimaenedeo ikiwemo ujenzi wa
majengo ya shule, zahananati pamoja na masoko.
Kwa upande wake
mwenyekiti wa mtaa wa Amani kata ya Tambukareli Bwana Kulwa Mazengo amesema pamoja na jitihada zinazofanywa na serikali
juu ya kutatua kero zao ikiwemo kero ya kukosekana kwa soko la kudumu, bado ameiomba
serikali kuwaboreshea miundombinu ikiwemo barabara katika eneo lao.
Hata hivyo jamii
imetakiwa kuendelea kuitunza miundombinu inayopelekwa na serikali katika maeneo
yao kwa mustakabali wa Taifa na kizazi kijacho.
Na
Victor Makwawa DODOMA FM
Comments
Post a Comment