
Serikali
kupitia wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto imejipanga
kuongeza juhudi za kufikisha elimu kwa wananchi ili kuzitambua njia za
kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa homa ya ini licha ya kuwepo kwa juhudi
zinazoendelea kufanyika.
Naibu
waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dr. Faustine Ndugulile
ametoa ufafanuzi huo leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge Mh.
Felister Aloyce Bura alietaka kujua Serikali inamkakati upi wa kutoa elimu kwa
wananchi ili kujiepusha na maambukizi ya ugonjwa huo.
Amesema
wizara ya afya kupitia vitengo vyake vya elimu kwa umma imekuwa ikiandaa majalinda pamoja na
machapisho mbalimbali kwa ajili ya kuifikishia jamii elimu ya kujikinga na
ugonjwa huo pamoja na kutembelea katika cliniki mbalimbali ili kuwafikia
wananchi kwa urahisi zaidi.
Amesema
virusi vya ugonjwa wa ini vimegawanyika katika makundi matano na tofauti yake
ni katika uambukizaji ambapo virusi vya kundi BC na D maambukizi yake
ni sawa na yale ya virusi vya ukimwi kupitia
njia ya kujamiiana, kuongezewa damu huku virusi vya kundi A na kundi E ikiambukiza
kwa njia ya unywaji wa maji yasiyokuwa safi na salama.
Akielezea
dalili za ugonjwa wa homa ya Ini Dr. Ndugulile amesema mgonjwa huanza kuonekana
akiwa na rangi ya njano katika ngozi na
macho, kujisaidia haja ndogo iliyo na rangi nyeusi, joto la mwili kupanda, kupata
mafua, kichwa kuuma, kupata kichefuchefu, kutapika pamoja na tumbo kuuma upande
wa juu kulia.
Na Pius Jayunga Bunge/DODOMA FM
Comments
Post a Comment