Serikali imesema
itahakikisha inajenga majengo mazuri katika majiji yote nchini ikiwemo jiji la
Dodoma ili kukabiliana na changamoto ya ujenzi holela .
Hayo yamebainishwa
leo na waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania MH Kassimu Majaliwa
wakati akifungua warsha ya siku mbili kwa wabunifu majengo na wakadiriaji yenye lengo la kutoa mafunzo ya kuendeleza ujenzi wa majengo ya
kitaalamu pamoja na miundo mbinu mipya.
Amesema kuwa wakati
serikali ikiendelea kujenga miundo mbinu mipya hasa katika jiji la dodoma bado pia itaendelea
kuyaboresha majengo yaliyopo katika majiji yote ambayo ni Mbeya, Mwanza Tanga
na Arusha na itahakikisha haifanyi makosa kama yaliyofanyika katika ujenzi wa
jiji la Dar es salaam.
Aidha ameongeza kuwa
kwa mwaka huu bodi ya wabunifu wa majengo na wakadiliaji wa majenzi itaandaa
michoro kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya kata katika ngazi za kata na amewataka
wataalu kusimamia kikamilifu ujenzi huo ili kupata majengo na vituo bora vya
afya nchini kote.
Kwa upande wake
waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Makame mbarawa amesema kuwa ili
kukabiliana na changamoto ya upungufu wa rasilimali fedha wizara imetenga kiasi
cha shilingo milioni 50 kwa ajili ya zoezi hilo kwa mwaka huu na katika bajeti
ijayo ya mwaka wa fedha 2018/19 jumla ya shilingi milioni 100 zimetegwa ili
kuondoa mapungufu yaliyopo.
Alfred
Bulahya DODOMA FM
Comments
Post a Comment