
Katika kipindi cha
mwezi June 2015 hadi Desemba 2017 Serikali imetumia kiasi cha shilingi bilioni
33.135 kulipa madai ya walimu wapatao
86,234 Nchi nzima.
Naibu Waziri ofisi
ya Rais tawala za Mikoa na Serikali za mitaa TAMISEM Mh. Josephat Kandege
ameyasema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge Hussen
Nassoro Amary aliyehoji ni lini walimu wataboreshewa masilahi yao na nyumba za
kuishi.
Amesema Serikali ya
awamu ya tano imedhamiria kuboresha masilahi ya walimu Nchini ikiwemo ujenzi wa
nyumba za walimu pamoja na miundombinu mingine ya shule na kwamba ili
kufanikisha swala hilo viongozi mbalimbali wakiwemo wabunge ni wadau wakubwa
katika kuunga mkono juhudi hizo.
Naibu Waziri huyo
amesema kupitia sheria namba 25 ya mwaka 2015 ilianzisha tume ya utumishi ya
walimu ili iweze kusimamia na kushughulikia masuala yahusuyo masilahi ya walimu
na katika kuhakikisha masilahi ya walimu yanaboreshwa na kero zao kuondolewa
jumla ya walimu 52 katika Halimashauri ya Wilaya ya Nyang’wale walilipwa jumla
ya sh. Milioni 99,685,990 za madai mbalimbali.
Mh. Kandege amesema
katika Mkoa wa Kagera una mahitaji ya vyumba vya madarasa 14,275 kwa shule za
msingi, mahitaji ya ofisi za walimu 1780, na katika shule za sekondari vyumba
vya madarasa vikihitajika 2,379, majengo ya utawala yakihitajika 212 changamoto
ambazo Serikali inaendelea kuzifanyia kazi kutokana na ongezeko la watoto
kuandikishwa shuleni.
Na
Pius Jayunga
Bunge/Dodoma FM
Comments
Post a Comment