Skip to main content

SERIKALI IMEANZA KUANDAA KITINI CHA MASUALA YA JINSIA

                                            Image result for Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jinsia Bi. Mboni Mgaza




Serikali imeanza mchakato wa kuandaa kitini cha masuala ya jinsia kuendeleza kasi ya utekelezaji wa mpango wa kitaifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Akizungumza katika kikao cha wataalam na wadau wa maendeleo ya Jinsia Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jinsia Bi. Mboni Mgaza amesema Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto umekithiri sana nchini  hivyo Serikali kuamua kutafuta njia tofauti za kupambana na tatizo hilo.

Amesema  lengo la kuandaa kitini cha kufundishia masuala ya Jinsia “ni kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto ambao utatoa uelewa kwa wadau wa maswala ya jinsia na maafisa Maendeleo ya Jamii kuanzia ngazi ya Mkoa, Halmashauri na kata ili kutoa elimu ya masuala ya Jinsia katika jamii.

Bi. Mboni amefafanua kuwa kwa mujibu wa takwimu ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 idadi ya wanawake nchini ilikuwa ni Milioni Ishirini na Tatu na Elfu Hamsini na nane Mia tisa Thelathini na tatu sawa na asilimia 51.3 ya watanzania na ndio wanaokumbwa na vitendo vya ukatili kwa kiasi kikubwa.

Amesisitiza kuwa kitni hicho kitazingatia masuala mbalimbali kama vile lugha na mazingira ya walengwa hasa wa vijijini ili kiweze kuleta matokeo mazuri katika kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto nchini.

Mariam Matundu                                                      Dodoma FM

Comments

Popular posts from this blog

MITI YA KIVULI MAARUFU KAMA PANGA UZAZI YAZUA TAHARUKI WILAYANI BAHI DODOMA

                                                  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bahi Jijini Dodoma Dk.Philipina Philipo amewatoa hofu wakazi   wa Wilaya hiyo juu ya taarifa za kuwepo kwa madhara katika miti ya kivuli maarufu kama PANGA UZAZI ambayo imezua hofu kwa wananchi hao. Hoja hiyo imeibuliwa katika kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo ambapo baadhi ya madiwani wameomba kupatiwa ufafanuzi kuhusu kuwepo kwa fununu kuwa mti huo una madhara na kuongeza kuwa baadhi ya wananchi wameanza kuikata wakihofia kupatwa na madhara hayo. Akitoa ufafanuzi kuhusu miti hiyo Mganga Mkuu wa Wilaya Dk.Philipina Philipo amesema hadi hivi sasa hakuna utafiti wowote uliofanyika na kubainisha kuwa mti huo hauna madhara hivyo wananchi hawana haja ya kuhofia chochote. Kutokana na Majibu hayo ya DK PHILIPINA yamepelekea kuibua kwa hoja nyingine kwa madiwani ambapo baadhi yao wametoa maoni tofauti tofauti juu ya ufafanuzi huo. Kufuatia hayo katibu  tawala msaidizi mkoa anayesh

YANGA KESHO KUJUA ANACHEZA NA NANI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

MAJINA ya vigogo wa soka Afrika, wakiwemo mabingwa wa Afrika 1998, Raja Casablanca yametawala katika orodha ya wapinzani wapya wa Yanga kwenye michuano ya Afrika. Yanga SC imeangukia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambako watamenyana na moja ya timu zilizofuzu hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo. Hiyo ni baada ya kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya sare ya 0-0 na wenyeji, Township Rollers Jumamosi jioni Uwanja wa Taifa mjini Gaborone nchini Botswana. Matokeo hayo yanamaanisha Rollers inakwenda hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza historia hiyo kwa ushindi wa jumla wa 2-1 uliotokana na matokeo ya mchezo wa                              kwanza Dar es Salaam Machi 6. Na Yanga SC itamenyana na moja ya timu zilizofuzu hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo, ambazo ni CR Belouizdad, USM Alger za Algeria, Al-Masry ya Misri, Djoliba ya Mali, Raja Casablanca, Enyimba ya Nigeria, SuperSport United ya Afrika K

MIKOA INAYOONGOZA KWA UKEKETAJI TANZANIA YATAJWA

Mila potofu   katika jamii ya kimasai imetajwa kuwa changamoto kwa maafisa ustawi wa jamii wa halimashauri ya wilaya ya Ngorongoro  kutokana na kukosa ushirikiano wa kutatua Tatizo la ukeketaji kwa jamii hiyo. Akizungumza na waandishi ya habari Afisa Ustawi Wa jamii Bwana ALOYCE  LOLIKISWALI katika semina iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sanyansi na Utamaduni UNESCO kwa lengo la kupinga ukeketaji wa wanawake amesema kukosekana kwa ushirikiano kwa jamii imekuwa ni changamoto ambayo imepelekea kushindwa kudhibiti ukeketaji pamoja na ukatili wa kijinsia. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Malaigwanan Bwana JOSEPH TIRIPAI amebainisha kuwa mila na desturi zao zitabadilika kulingana na wakati lakini watahakikisha wanalinda watoto wanaozaliwa kutokeketwa na kusisitiza elimu kuendelea kutolewa hususani shuleni. Katika hatua nyingine mratibu wa afya ya mama na mtoto ameeleza kuwa wanawake wajawazito waliokeketwa wanalazimika   kujifugua kwa upasuaji na