Elimu ndogo dhidi
ya watendaji pamoja na kutokuwepo uaminifu na migogoro ndani ya vyama vya
msingi vya ushirika imetajwa kuwa chanzo cha kupelekea wakulima kuuza mazao yao
kwa walanguzi badala ya kuuza katika vyama hivyo.
Kauli hiyo inakuja
baada ya serikali kutakiwa kuweka mipango mikakati mizuri ya kuhakikisha
mkulima anauza mazao yake katika vyama vya msingi na kuepukana kuwauzia
walanguzi jambo ambalo linachangia kutonufaika na mazao yake.
Akizungumza na
Dodoma FM juu ya suala hilo mkurugenzi wa shirika la usimamizi na ukaguzi wa vyama
vya msingi COASCO Tanzania bwana SAAD WADAA amesema kuwepo na watendaji
wenye elimu ndogo katika vyama hivyo husababisha utendaji mbaya katika kuhudumia wahitaji
huduma na hivyo chama kubezwa na wananchi
kingine ikiwa ni baadhi ya watendaji kuingia katika nyazfa za uongozi
kwa maslahi binafsi.
Bwana WADAA amesema
jambo jingine linalofanya wakulima wasiuze mazao yao katika vyama hivyo ni
kuwepo kwa migogoro baina ya viongozi jambo ambalo amesema hapo nyuma lilikuwa
likichangiwa na maswala ya kisiasa.
Aidha mkurugenzi huyo amesema wao wakiwa wakaguzi na wasimamizi wamekuwa wakitatua migogoro ambayo
iko chini yao kwa mjibu wa sheria huku migogoro inayohusiana na ubadhirifu wa
fedha ikitatuliwa na vyombo vingine kama
polisi na Takukuru.
Hata hivyo amewataka wananchi kuwa makini wanapofanya uchaguzi wa viongozi wa
vyama vya msingi kwa kuzingatia sifa alizonazo mhusika ili kuleta ufanisi wa
kazi katika vyama hivyo jambo ambalo litaepusha migogoro isiyo ya lazima.
Na
RWEIKIZA KATEBALIRWE DODOMA FM
Comments
Post a Comment