MKUU wa mkoa wa Dodoma,Dk.Binilithi Mahenge
amewahakikiasha wafanyakazi wote kuwa utaratibu wa kuunganisha mafao yao upo
vizuri na hakuna mafao ya wafanyakazi yatakayopotea kutokana na mafao hayo
kupelekwa katika mfuko husika.
Akizungumza katika maadhimisho ya sherehe za Wafanyakazi (Mei
Mosi zilizopambwa na maandamano mbalimbali ambayo yamefanyika jijini Dodoma
katika uwanja wa jamuhuri huku kauli mbiu ikiwa ni kuunganishwa kwa mifuko ya
hifadhi ya jamii nchini ukilenga kuboresha mafao ya wafanyakazi.
DK BINILITH MAHENGE Amesema ujumbe huo una lengo la
kuijulisha serikali kama msimazi mkuu wa sheria ya ajira ikiwemo haki za
wafanyakazi na moja ya sera ya serikali imelenga kutoa haki kwa wananchi wote
pamoja na watumishi.
Akisoma risala kwa niaba ya wafanyakazi mjumbe
wa kamati ya utendaji TUICO mkoa GODFREY NDOSHI, amesema kuwa
wafanyakazi wanakabiliana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa na mishahara midogo ambayo wakati mwingine wafanyakazi wanashindwa kufikia malengo.
wafanyakazi wanakabiliana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa na mishahara midogo ambayo wakati mwingine wafanyakazi wanashindwa kufikia malengo.
Katika hatua nyingine NDOSHI,
ameongeza kuwa serikali inatakiwa
kuwawajibisha waajiri ambao wamekuwa na tabia ya kuchelewesha makato ya watumishi au kutolipa kabisa katika mifuko ya jamii jambo ambalo linasababisha kuwepo kwa malalamiko kati ya mfuko, mwajiri na mwajiriwa.

Nchini Tanzania Maadhimisho ya Mei Mosi kitaifa yameadhimishwa katika mkoa wa iringa.
Na,Mindi
Joseph Dodoma
FM
Comments
Post a Comment