Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dokta
John Pombe Maguful ileo tarehe 25 Mei, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Wenyekiti
watatu wa Jumuiya za CCM, IkuluJijini Dar es Salaam.
Wenyeviti hao ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi
Tanzania Ndg. Raymond Mndolwa, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Ndg. Gaudensia Kabaka na Mwenyekiti
wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)
Ndg. Kheri James.
Baada ya mazungumzo hayo viongozi hao wamesema wamekutana
na Rais Magufuli na kumueleza kuhusu maendeleo
ya Jumuiya zao na kumpa salamu kutoka kwa Rais wa Afrika Kusini Ndg. Cyril
Ramaphosa na Rais wa Zimbabwe Ndg. Emmerson Mnangagwa pamoja na viongozi wa vyama
tawala vya ANC cha Afrika Kusini na ZANU-PF cha Zimbabwe ambavyo ni vyama rafiki
vya CCM.
Katika hatua
nyingine Rais Magufuli
amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu na Mwenyekiti Mstaafu
wa CCM Ndg. Benjamin William Mkapa na Makamu Mwenyekiti wa
CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula, Ikulu
Jijini Dar es Salaam.
Comments
Post a Comment