Rais wa Jamhuri ya muungano wa
Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amesema lengo la serikali kuwekeza katika
ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo Nchini ni kujenga mazingira mazuri ya
kuboresha masilahi ya watumishi wa umma katika siku za usoni.
Rais
Magufuli ametoa kauli hiyo leo katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi MEI
MOSI yaliyofanyika kitaIfa katika Mkoa
wa Iringa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Waziri mkuu
Kasimu Majaliwa.
Amesema
fedha ambazo zimekuwa zikitolewa na Serikali kufanikisha mpango wa elimu bila
malipo kwa wanafunzi kiasi cha shilingi bil. 23.8, mikopo kwa wanafunzi wa
elimu ya juu kiasi cha shilingi bil. 483 inalenga kunufaisha pande zote kuliko
kutumia fedha hizo kujiongezea mishahara inayonufaisha upande mmoja wa
watanzania.
Katika
hatua nyingine Rais Magufuli amesisitiza suala la malipo kwa mfanyakazi pale anapohamishwa
kituo cha kazi kupatiwa stahiki zake na kwamba zoezi hilo linapaswa kusimamiwa
kikamilifu na waajiri katika maeneo yote Nchini.
Kwa
upande wake katibu mkuu wa TUCTA Nchini Dr. Yahaya Msigwa amesema chama cha
wafanyakazi Nchini TUCTA hakita kubali kuwavumilia wafanyakazi wazembe, wavivu
na wale wasio kuwa na nidhamu na kwamba vitendo vya rushwa vitaendelea kukemewa
miongoni mwa wafanyakazi.
Na Pius
Jayunga Dodoma FM
Comments
Post a Comment