
Rais
wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Mgufuli amesema Serikali imejitahidi
kuongeza bajeti ya Wizara ya afya kwa sehemu kubwa kila mwaka kwa lengo la
kuboresha huduma za afya na kuwafikia wananchi kwa urahisi.
Rais
Magufuli ameyasema hayo leo wakati akiweka jiwe la msingi la Ujenzi wa
hospitali ya Wilaya ya Kilolo iliyopo Mkoani Iringa na kueleza kuwa jitihada
hizo ni utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi kuboresha huduma za afya
Nchini.
Amesema
kwa mwaka 2015/16 bajeti ilikuwa Trilioni 1.8 na mwaka 2016/17 bajeti
ikaongezeka hadi kufikia Trilioni 2.2 zote zikipelekwa katika sekta ya afya
ambapo kwa sasa vituo vya afya zaidi ya 208 vimejengwa na vingine
vikikarabatiwa huku mkakati uliopo ikiwa ni kujenga hospitali za wilaya 67.
Aidha
Rais Magufuli ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wananchi kujiunga katika
mifuko ya bima ya afya ili kunufaika na huduma za matibabu pale mwanachama
anapougua ikiwa ni pamoja na Wizara ya afya kuendelea kuhamasisha wananchi
kujiunga kwa wingi ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya.
Kwa
upande wake Waziri wa Tamisem Mh. Seleman Jafo amesema tayari kamati ya Bunge
imekwisha fanya ziara ya kukagua ujenzi wa Hospitali hiyo na kurizishwa na
hatua za ujenzi wake na baada ya kukamilika ujenzi wa Hospitali hiyo itakuwa
msaada mkubwa kwa wakazi wa Wilaya ya Kilolo.
Na Pius Jayunga Dodoma FM Radio
Comments
Post a Comment