
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ameagiza fedha kiasi
cha sh. bil. 2 zilizoelekezwa katika chuo kikuu cha Dar es salaam zitumike
kujenga mabweni ya chuo kikuu cha Sokoine kilichopo Mkoani Morogoro.
Rais
Magufuli ametoa maagizo hayo leo akiwa Mkoani Morogoro wakati akizungumza na
wananchi pamoja na wanafunzi wa chuo kikuu cha Sokoine baada ya kupokea
malalamiko ya wanafunzi hao likiwemo suala la upungufu wa mabweni hatua
inayolazimu wengi wao kuishi mbali na eneo la chuo.
Rais
Magufuli amesema pamoja na changamoto zilizowasilishwa na wanafunzi hao bado Serikali
inatambua mchango wa chuo hicho katika kuboresha sekta ya kilimo Nchini na
kuagiza fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni. 2 zitumike kwa ujenzi wa mabweni
ili kuondoa.
Katika
hatua nyingine Rais Magufuli ameonesha kufurahishwa na hatua zilizofikiwa na
chuo cha Sokoine ikiwemo kufanya utafiti wa panya kugundua mahali ambapo
limefichwa bomu na kuahidi kuongeza idadi ya trekta zipatazo kumi chuoni hapo
kwa lengo la
Kwa
upande wake Waziri wa elimu sayansi na teknolojia Prof. Joyce Ndalichako
amesema chuo hicho kimefanikiwa kuvumbua mbegu za matunda aina ya papai zaidi
ya 4000 zenye uwezo wa kukomaa na kutoa matunda ndani ya miezi mitano, mbegu
zingine ikiwa ni mpunga pamoja na maharage.
Na Pius Jayunga Dodoma FM
Comments
Post a Comment