OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU IMETOA MAFUNZO KWA WAANDAAJI NA WATUMIAJI WA TAKWIMU ILI KUBORESHA UTOAJI TAKWIMU SAHIHI

Shirika la umoja wa mataifa linalojihusisha na usawa wa
kijinsia na maendeleo kwa wanawake lipo
katika mpango wa kuendeleza TAKWIMU za kijinsia likiwa na lengo la kufahamu idadi
ya wanawake pamoja na wasichana waliopo kote nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma Katika
Ofisi za CAG kupitia Warsha iliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu muwakilishi
kutoka shirika hilo Bi. USU MARYA amesema mpango huo unaenda sambamba na
malengo yaliyopo kwenye mkakati wa nchi wa miaka mitano ambao una lengo la
kuiendeleza nchi kwa kufahamu Takwimu katika sekta mbalimbali nchini.
Aidha Bi. USU amesema kuwa kuna haja kubwa ya kuweka
mikakati ya kufanya uchambuzi wa ziada
ambao utasaidia kupata idadi kamili ya wanawake wa vijijini na mijini pamoja na
wanaume ili kusaidia Taasisi pamoja na Wizara husika kujua Takwimu za kijinsia.
Nae Meneja wa Takwimu za Mazingira na Uchambuzi ambae pia ni
mshirika wa uratibu wa utekelezaji wa Takwimu kwa ajili ya kupima utekelezaji
wa mpango wa pili wa maendeleo ya taifa BI. RUTH MINJA amesema ofisi ya Taifa
ya Takwimu inashirikiana na wadau ili
kutoa Takwimu zitakazosaidia mipango mingine ya maendeleo kwa jamii.
Ukusanyaji wa Takwimu katika sekta mbalimbali ni moja ya sababu
inayopelekea kuwepo kwa maendeleo katika sekta husika pamoja kukua kwa uchumi
wa nchi kwa kufahamu idadi na malighafi zilizopo nchini.
Na ANIPHA RAMADHANI DODOMA FM
Comments
Post a Comment